Leo Janaury 7, 2019 Kundi la Wanajeshi nchini Gabon limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya Serikali katika Taifa hilo la Afrika Magharibi.
Wanajeshi wenye vifaru na magari ya kivita wapo katika doria maeneo mbalimbali nchini humo na katika barabara za Mji mkuu Libreville. Shirika la habari la AFP limesema milio ya risasi imesikika jijini humo.
Amri ya kutotoka nje imetangazwa.
Rais wa nchi hiyo Bongo amekuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miezi miwili, akipata matibabu nchini Morocco kutokana na maradhi ambayo hayajatangazwa baada ya kuugua akiwa ziarani Saudi Arabia.
KIZAAZAA CHA RC MWANRI “ITALIWA MBELE YA MACHO YAKO, ROGENI KIJIJI KIZIMA”