Mwalimu Christopher Mwakasege amezungumza kwa mara ya kwanza juu ya kifo cha Mtoto wake Joshua ambaye alifariki siku ya Alhamis Saa mbili usiku nakusema katika hali ya kawaida ya kibinadamu asingeweza kuendelea na Semina.
Nanukuu maneno ya Mwakasege aliyoyaongea leo akifunga Semina mkoani Mbeya “Alhamisi usiku tulifiwa na Mtoto wetu Joshua, alifariki ghafla, halikuwa jambo lepesi kwamba tuendelee na semina au tusiendelee, kwa jinsi ya binadamu halikuwa jambo rahisi kuendelea na semina. Biblia inatuambia tuwe tayari wakati unaofaa na usiofaa”. –Mwakasege
Rais Magufuli “Namalizia December nahamia Dodoma, nayoyafanya Tanzania ni kumuenzi Nyerere” (+video)