Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe ametoa agizo la kukamakatwa kwa Mwekezaji wa Kampuni ya Greenmil kwa madai ya kudaiwa na Vijiji 23 jumla ya Milioni 339 za maendeleo alizokubaliana na wananchi hao.
Awali mwekezaji huyo alimwandikia barua Mkuu huyo wa Wilaya ya kutaka kumsafisha ndani ya siku saba na endapo hatafanya hivyo atampeleka Mahakamani.