Baada ya Wazazi wa Mtoto aliefariki kwa kudaiwa kuchapwa viboko na Mwalimu wake kugoma kuchukua Mwili na kwenda kuuzika Mkuu wa wilaya Bukoba na RPC mkoani Kagera wametoa maagizo yao.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Augustine Ollom amesema tayari amewasiliana na Mganga Mkuu wa mkoa na wataunda jopo la Madaktari wataalam ili warudie vipimo katika Mwili wa Mwanafunzi.