Feb 14,2019 Katika kuadhimisha siku ya wapendano duniani maarufu kama ‘Valentine’s Day’ Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) imewakutanisha wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika utendaji kazi wa kampuni hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Februari 14, 2019 Mwenyekiti wa wanawake wa SBL, Anitha Rwehumbiza amesema lengo kubwa ni kuwainua wanawake ndani na nje ya ofisi kupitia jukwaa maalumu lijulikanalo ‘SBL spirited women’.
Hafla hiyo imefanyika katika Makao Makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo Chang’ombe jijini hapa pamoja na matawi yaliyopo mikoa ya Mwanza na Moshi.
“Lengo ni kuwainua wanawake katika nyanja tofauti sio tu katika kazi lakini pia nje ya ofisi na kwa mwaka huu tumeona tujumuike pamoja tuonyeshe upendo wetu kwa wanawake wote wa Serengeti na kuwashukuru wanawake kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kuendeleza kiwanda chetu,” Rwehumbiza.
Rwehumbiza amesema katika siku hiyo ya wapendanao Kampuni ya Serengeti inawakumbusha watanzania kuzingatia unywaji wa kiistaraabu.
“Kwa wateja wetu tunawashukuru sana kwa kuwa pamoja na sisi kwasababu uwepo wetu unategemea zaidi wafanyakazi na vilevile wanywaji wetu wakubwa,” Rwehumbiza
Wanawake hao walionyesha umaridadi kwa kuvaa mavazi ya rangi nyekundu ambayo huvaliwa katika siku hiyo na kukabidhiwa kinywaji maalumu kijulikanacho kama ‘Baileys’ kinachotengenezwa na kampuni mama ya Diageo na kusambazwa na kampuni ya bia Serengeti.
MAPYA HAYAISHI KWA RC MWANRI “NINA MTAZAMA KWA DHARAU, NITAMZIBUA”