Mwenyekiti wa zamani wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya kusambaza dawa bandia za UKIMWI wamepelekwa gerezani baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusema haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Hata hivyo Mahakama imeutaka upande wa mashtaka kuhakikisha December 15, 2017 unawasilisha taarifa Mahakama Kuu kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi au kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili kesi hiyo isikilizwe na taratibu za dhamana ufanyike.
Akitoa uamuzi Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa amesema amepitia hoja za upande wa mashtaka na utetezi kuhusu Mahakama hiyo kama ina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo ama la na kubaini kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo.
Madabida na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi ikiwamo kusambaza dawa bandia za kufubaza virusi vya Ukimwi ‘ ARV’s ‘ na kusababisha hasara ya Sh 148 milioni.
Ulipitwa na hii? SIKU YA II: Kesi ya M/kiti wa zamani wa CCM Ramadhan Madabida