Katika kuelekea uchumi wa kati unaonaendeshwa na viwanda nchini, serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango inatoa mikopo kwa wajasiriamali na watanzania wote ili kuwawezesha kukua kiuchumi kupitia mfuko wa ‘Self Micro Finance’.
Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa Self Micro Finance Mudith Cheyo, ambao ni mfuko wa serikali ulioanzishwa mwaka 2000 na tayari umehudumia nchi nzima na ina ofisi saba ambazo zinatoa huduma kikanda.
Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni, ” Zanzibar, Dodoma, Mwanza, Kahama, Mbeya, Arusha na Dar es salaam”.
Naye Mkurugenzi wa Mkopo SELF MF, Santiel Yona amesema kuwa wanatoa mikopo kwa Watanzania wote bila kujali matabaka isipokuwa ni kuhakikisha uzoefu wa biashara kwa mhusika pamoja na uhalali wa biashara ile ikiwemo kuwa na leseni ya biashara.