Basi la Mwendokasi lililokuwa linatokea Mjini kwenda Kimara Mwisho limeteketea kwa moto eneo la Kimara Mwisho DSM usiku huu, hakuna madhara yoyote yaliyojitokeza kwa Binadamu, Kaimu Kamanda wa Polisi Kinondoni amesema bado chanzo cha ajali hakijajulikana hadi pale uchunguzi utakapofanyika.
“Gari ya mwendokasi ilikuwa mbele yetu tukaona inavuja mafuta, Dereva alipata taarifa akashuka akaenda kuichungulia akaendelea na safari ila hatua chache kabla hajafika kituoni gari ikaanza kuwaka moto” – Rajabu Athmani (Shuhuda)