Viongozi wa Pakistan wamemchagua Jaji Mstaafu Nasirul Mulk kuiongoza nchi hiyo kama Waziri mkuu wa mpito atakayesimamia uchaguzi mwezi July mwaka huu.
Kiongozi wa upinzani Khursheed Shah amesema kuwa Nasirul Mulk atakuwa waziri mkuu wa muda.
Mulk, mwenye umri wa miaka 68, alistaafu kama Jaji mkuu wa Pakistan August 2015.
Awamu ya serikali ya sasa inatarajiwa kukamilika wiki hii, na uchaguzi kufanyika July 25.
Katiba ya Pakistan inampa waziri mkuu na kiongozi wa upinzani mamlaka ya kuchagua mtu asiyeegemea upande wowote kutawala mpaka uchaguzi utakapofanyika.