Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla amejibu kile alichoandika Waziri wa Mazingira, January Makamba juu ya utaratibu mpya wa kutumia magari maalumu ya umeme (Cable Cars), kwa ajili ya watalii wanaotembelea mlima Kilimanjaro.
Waziri Kigwangalla amandika katika Twitter yake “Hivi kuna nchi ngapi zimeweka Cable Cars kwenye milima yake?, hizi haziharibu mazingira?, Cable inapita juu inaharibu mazingira gani?. Zaidi ya hekari 350,000 za misitu zinapotea kila mwaka nchini, ipi ni hatari kubwa?, watu wa mazingira wamechukua hatua gani zaidi ya makongamano tu?”,
Hivi karibuni wakati TANAPA ilieleza mpango wake wa kuja na namna mpya ya usafiri kwa watalii wanaotaka kwenda kutembelea mlima Kilimanjaro.
Waziri Makamba aliandika“Inabidi watu wa Mazingira tupitishe na kutoa cheti kwanza kabla hawajaanza. Na tutafanya ‘studies’ ili kujua madhara kwa mazingira na uthabiti wa ‘mitigation measures“,