Naibu Spika Dk. Tulia Ackson amesema yupo tayari kuichangia timu ya Young African kutokana na ukata wa fedha unaoikabili timu hiyo kongwe kwa sasa.
Ameyasema hayo alipoitisha mkutano na waandishi wa habari leo nyumbani kwake Jijini Mbeya kuzungumzia kuhusu Tulia Marathon ambayo itafanyika Mei 4 mwaka huu, ambapo amesema akiwa kama Kiongozi ameyapokea maombi ya timu hiyo kongwe na yupo tayari kuisaidia kwani wapo Viongozi wengi walioanza zoezi hilo wakiwemo Wabunge.
Aidha amewataka Wanambeya kushiriki kwa wingi katika mashindano ya Tulia Marathon ambayo yanatarajiwa kuanza mapema tarehe 4 mwezi Mei 2019.
Pia alitumia nafasi hiyo kuwaomba mashabiki wa Simba na Mbeya City kubaki had tarehe 4 ili kuweza kushiriki mashindano hayo ambapo timu hizo zinatarajiwa kucheza Mei 5 mwaka huu katika Viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya.