Leo November 1, 2019 Mtoto wa miaka 12 ameshinda nafasi ya kusoma Chuo Kikuu masomo ya Utawala wa Umma anaitwa Viemens Bamfo, ni mtoto mdogo zaidi kati ya wanafunzi 3000 waliodahiliwa katika Chuo Kikuu cha Ghana.
Alishinda mtihani wa majaribio kwa alama za juu baada ya kufundishwa na baba yake Robert Bamfo nyumbani.
Ameiambia BBC kuwa anatamani kuwa na kazi ya juu kabisa nchini Ghana.
”Ninataka kuwa Rais wa Ghana, ninataka kupeperusha bendera ya Ghana na kuifanya Ghana kuwa nchi huru ya kweli kama ilivyo Marekani, Uingereza, China na nchi nyingine.”
Ana matumaini ya kusoma Sheria ya Katiba, Mifumo ya Kisiasa, masuala ya Uongozi, Uchumi na Utunza fedha.
MWANASHERIA “MAKONDA AFUATE UTARATIBU, HAKUNA KOSA LOLOTE, PICHA YA RAIS SI NEMBO YA TAIFA”