Mahakama ya Wilaya ya Gairo imemuhukumu kifungo Cha miaka 30 jela makazi wa Chakwale, Michael Mchanjale (31) baada ya kumtia hatia kwa kosa la kumbaka mtoto wa shemeji yake mwenye umri wa miaka 15 ambaye ni mwanafunzi wa kidato Cha kwanza.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi Mwanadamizi Mfawidhi, Irene Lyatuu alisema mshitakiwa huyo ametiwa hatia kwa kosa hilo la ubakaji ambapi anahukumiwa kwenda jela miaka 30, huku rufaa ikiwa wazi endapo kama muhukumiwa hajaridhika.
Hakiku Lyatuu alisema mshtakiwa anadaiwa alitenda kosa hilo Septemba 22, 2023 baada mlalamikaji kufika nyumbani kwa mtuhumiwa ambaye ni baba yake mdogo baada ya mama yake wa kambo kumfukuza nyumbani baada ya Binti huyo kuchelewa kurudia ambapo baada ya kufika hakufanikiwa kumkukuta mama yake mdogo badala yake alimkuta mtuhumiwa ( baba yake ndogo) majira ya saa tatu usiku.
Hakimu Irene alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa kinyume Cha Sheria namba 130 (1)(2) (e) na kifungu cha Sheria 131 kifungu cha adhabu (1) kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya 2022 .
Alisema baada ya Mwezi mmoja msichana huyo aligundulika kuwa na ujauzito na alipoulizwa alidai baba yake mdogo (mtuhumiwa) Michael Mchanjale ndiye aliyembaka usiku na kumtishia asiseme kwa mtu yoyotela sivyo atamua
Hakimu Irene alisema katika kesi hiyo jumla ya mashahidi 6 walitoa ushahidi upande wa jamhuri akiwemo mlalamikaji pamoja vielelezo vitatu ikiwemo Cha daktari ambacho kilionesha msichana huyo aliingizwa kitu chenye ncha kali sehemu za siri na kuondoa nyama nyama laini.
Akitoa ushahidi mbele ya mahakama mlalamikaji anasema siku ya tukio baba yake mdogo (mtuhumiwa) alimgongea mlango majira ya usiku na alipoingia ndani alizima taa kisha kumvua nguo na kumziba mdomo badae kuchukua uume wake na kuingiza kwenye uke wake na alitumiwa dakika 20 huku akisikia maumivu makali kwani alikua ajawahi kuingizwa kitu chochote sehemu zake za siri (uke).
Hakimu Irene anasema mtuhuma huyo amefikishwa kwa makosa mawili ikiwemo la kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi ambapo Mahakama hiyo imetia hatia kwa kosa moja la kubaka huku ikimuachia huru kwa kosa la kumpa ujauzito hadi ushahidi utakapo wasilishwa ikiwemo vipimo vya DNA.
Kesi hiyo iliendeshwa na Wakili wa Serikali, Elias Masini kwa upande wa Jamhuri huku mtuhumiwa akijitetea mwenyewe