Viongozi wa Taliban wamepiga marufuku uwepo wa midoli inayofanana na Binadamu madukani ambayo huvalishwa nguo na kutumika kuvutia biashara nchini humo huku wakisisitiza kwamba midoli ni kama sanamu na kwamba imani za Kiislamu zinakataza Watu kuabudu sanamu.
Baada ya malalamiko ya Wafanyabiashara wengi kuhusu agizo la kuiondoa Viongozi wa Nchi hiyo ambao ni Taliban waliagiza vichwa vya midoli vinyofolewe na vibaki viwiliviwili tu lakini hilo nalo likapingwa na Wafanyabiashara.
Baada ya mvutano huo imembidi Waziri mwenye dhamana kuwaambia Wafanyabiashara hao kwamba kama wataiacha midoli ikiwa na vichwa basi vichwa hivyo visitiriwe kwa kuvalishwa Hijab.