“Ada ya kusafisha ya dola 50 sawa na 125,000 za kitanzania kwa kila mtu kwa tukio lolote linalotokea kwa sababu ya ulevi,” inasomeka barua kwenye menyu kwenye mgahawa wa California.
Shughuli ya wikendi ambapo marafiki hukusanyika ili kula mseto/aina mbalimbali za vyakula na hasa kiamsha-kinywa na chakula cha mchana, kutazama maisha yao na, wakati mwingine, kunywa pombe kupitiliza na kusababisha uharibifu basi watagharamika kulipia hasara itakayotokea.
Sasa baadhi ya migahawa ya California inajaribu kuzuia ulevi huo wa kupindukia kwa kuwatoza wote watakao zidisha vilevi na kufanya vurugu.
Sehemu tatu maarufu za chakula cha mchana katika eneo hilo zimekuwa zikishughulika na watu wanaokunywa pombe kupita kiasi na hatimaye kuchafua – wakati mwingine kwenye meza zao kwenye chumba cha kulia chakula.