Miili ya wanafunzi wawili kati ya wanne waliozama katika tukio la mtumbwi kuzama katika mto luiche Mkoani Kigoma imepatikana Feb 25, 2023 asubuhi na kuhifadhiwa katika hispitali ya Rufaa ya mkoa Maweni.
Kaimu kamanda wa jeshi la Zimamoto na uokoaji Inspekta Jacob Chacha ametaja majina ya wanafunzi hao kuwa ni Zabibu Jumanne(8) darasa la 2 na Ramadhani Nkwila (12) darasa la tano.
Zoezi la uokoaji wa Watoto hao limeendelea leo asubuhi baada ya siku ya jana kushindwa kufanyika,majira ya asubuhi na mapema miilia hiyo imeanza kuonekana ikielea katika mto Luiche karibu kabisa na Ziwa Tanganyika.
Miili ambayo haijapatikana ni hadi sasa ya watoto wawili Ashura Haruna wa darasa la kwanza na Tatu Sanaari(6) wa Darasa la kwanza,Juhudi za uwatafuta zinaendelea na vikosi vya uokoaji kutoka mkoani Kigoma.