Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema wataendelea kuhakikisha wanaweka mazingira bora na wezeshi kwa timu ya riadha ya Jeshi la Polisi ili kufanya vyema katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na kuutangaza utalii wa Nchini.
SACP Masejo ameyasema hayo leo Disemba 11, 2024 katika tafrija fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza wanariadha hao mara baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kuwapandisha vyeo wanariadha watatu waliofanya vizuri zaidi katika mashindano ya kimataifa toka nchi mbalimbali.
Kamanda wa Masejo amebainisha kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo litahakikisha linawatuhumia vyema wanariadha hao katika kutangaza Taifa na vivutio vilivyopo nchini kupitia mashindano watakayoshiriki.
Kambi ya Timu hiyo ipo mkoani Arusha ambapo inajumuisha wanariadha wa Jeshi la Polisi toka mikoa mbalimbali hapa Nchini.