Leo February 20,2020 Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema mpango wa Serikali ya Afrika Kusini kuchukua ardhi bila kutoa fidia ni hatari kwa uchumi wa nchi hiyo.
Afrika Kusini ipo katika majadiliano ya kubadilisha Sheria na kuruhusu Serikali kuchukua mali binafsi bila kutoa fidia, kwa mujibu wa takwimu, takriban 72% ya mashamba yanamilikiwa na Wazungu, ambao ni 9% ya Raia wa nchi hiyo.
Pompeo amesema Uchumi wa Afrika unahitaji Utawala wa Sheria wenye nguvu, heshima kwa umiliki na Sheria zinazochochea uwekezaji.
Hii sio mara ya kwanza kwa Utawala wa Rais Trump kuingilia kati masuala ya ardhi katika nchi hiyo. Mwaka 2018, Trump alidai Serikali ya Afrika Kusini inashikilia mashamba na wakulima wengi wanauawa.
PROF. TIBAIJUKA AWATANGAZIA WANANCHI WAKE KUSTAAFU “SITOGOMBEA UBUNGE”