Waziri wa Nishati January Makamba amesema kukamilika na kuanza kufanya kazi kwa Bomba la mafuta la Tanzania Zambia Mafuta Pipeline (TAZAMA) litawanufaisha zaidi Watanzania wanaopatikana Mikoa ya kusini ambayo bomba hilo la mafuta limepita kuelekeza Zambia hao watapata mafuta kwa unafuu ukilinganisha na mikoa mingine.
Waziri Makamba amesema gharama za usafirishaji wa mafuta zitapungua zaidi kwa mikoa hiyo na kusema >>’Tutaisaidia Mikoa ya kusini mwa Tanzania kupata mafuta kwa bei nafuu kwa sababu kwenye mpango mpya kutakua na matoleo ya kushusha mafuta katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Mbeya mpaka Songwe maana yake barabarani kutakua na Magari machache na gharama za mafuta zitakua nafuu zaidi ndio maana miradi hii tunaipenda sababu inaenda kusaidia Watanzania wengi’ – Waziri Makamba.
Waziri Makamba amesema haya ni mashirikiano mazuri kati ya nchi zetu hizi na pia ni mwendelezo wa mahusiano mema unaofanywa na Viongozi wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Hakainde Hichilema, Rais wa Jamhuri ya Zambia kama yalivyoasisiwa na Viongozi wetu wa kwanza Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere na Hayati Kenneth Kaunda.