Mikopo ya zaidi ya milioni 516 imeweza kutolewa na Halmashauri ya Ushetu kwaajili ya wanawake,Vijana na wenye ulemavu katika kipindi cha mwaka 2021/2022.
Mikopo hiyo imetolewa kwa vijana katika vikundi 14 yenye thamani ya Shilingi milioni 123,800,000,wanawake ni shilingi milioni 379,720,000 katika vikundi 41 na kwa upande wa watu wenye ulemavu imetolewa shilingi 13,100,000 katika vikundi vitano.
Takwimu imetolewa katika mkutano wa mwaka mmoja wa ubunge wa mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani uliofanyika katika Kijiji cha Iramba Kata Igwamanoni ambapo ameongeza kuwamiradi ya maji iliyotekelezwa na kukamilika kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2021/2022 kwa gharama ya shilingi 3,368,325,037.01 ni pamoja na mradi wa maji wa vijiji vya (Mpunze, Sabasabini na Iponyanholo), Vijiji vya (Igunda na Mhulidede), na kijiji cha Nyankende pamoja na kijiji cha Kisuke.
Kwenye sekta ya elimu Mbunge Cherehani amesema kuwa kupitia serikali kuu na wadau Halmashauri imeweza kujenga vyumba 104 vya madarasa ya Sekondari kwa gharama ya shilingi 2,080,000,000.00 ikiwa ni pamoja na kujenga shule mpya ya sekondari iliyopo kijiji cha Mwadui.
Katika sekta ya kilimo Halmashauri ya Ushetu imepokea mbolea ya ruzuku kwa ajili ya zao la tumbaku Tani 15,000 sawa na shilingi 21,000,000.00, NPK Tani 18,000 sawa na shilingi 55,000,000,000.00.
Kwenye zao la Pamba wakulima wamegawiwa mbegu za zao hilo zenye thamani ya shilingi Bilioni 6.2 hali itakayopelekea kuongeza wastani wa uzalishaji wa zao hilo kutoka milioni 8 vilivyokuwa mwaka 2021/2022 hadi Tani milioni 18 kwa mwaka 2022/2023.