Leo January 8, 2018 Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESBL) imeshindwa kutekeleza kampeni ya ukaguzi wa wanufaika wa mikopo na wadaiwa sugu wa bodi hiyo baada ya kuzuiwa katika Ofisi za Puma Energy jijini Dar es Salaam.
HESBL walizuiwa kutekeleza kampeni hiyo leo baada ya Meneja Rasilimali watu wa Puma Energy kukataa kuonana na uongozi wa bodi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya tukio hilo, Mkurugenzi wa Urejeshwaji mikopo Fidelis Joseph amesema, Puma Energy ni miongoni mwa makampuni yaliyopo kwenye orodha ya walioshindwa kutekeleza sheria ya mikopo.
Pia wamekuwa wakiwakata fedha waajiriwa wao lakini hawazirejeshi fedha hizo kwa bodi kwa wakati kama ambavyo sheria inatamka.
“Tumefika hapa kwa ajili ya kukagua lakini Meneja wao amekataa na sababu anazozitoa ni kwamba kwanini tumekuja na watu ambao sio wafanyakazi wa bodi, wakati sheria inaturuhusu kuja na mtu yeyote hata kama Polisi,” -Fidelis Joseph
Kutokana na hatua hiyo, Joseph amesema ni dhahiri serikali na wanafunzi wanaosomeshwa kwa mikopo wamedharauliwa, hivyo sheria itachukua mkondo wake.
FEDHA ZILIZOKUSANYWA NA TRA KWA NUSU YA MWAKA WA FEDHA 2017/18