Katika kuendelea kutokomeza vitendo vya Ukatili wa kijinsia ndani ya kata zetu na maeneo mbalimbali ya Mikoa Wadau mbalimbali wa mashirika wamejitokeza katika kukabiliana na Matukio hayo hasa kumsaidia mtoto wa kike ambaye amekuwa mstari wa mbele katika vitendo hivyo.
Akitolea ufafanuzi Afisa Mtendaji wa Kata ya Kasamwa Ndg .Victor Bashingwa amesema kata yake imekuwa ikikumbwa na matukio ya aina hiyo ambayo yamekuwa si kivutio kwa Serikali na ili kukabiliana nayo wamekuwa wakiunda kamati katika kuhamasisha na kutoa Elimu juu ya vitendo vya ukatili hasa kwa mtoto wa kike ambaye amekuwa akizungumzwa kila eneo.
“Katika kata hii pamekuwa kuna matukio mbalimbali ya ukatili ambayo yana husisha mtoto na lakini vilevile na wakina Mama kama tunavyofahamu kutokana na mila zetu lakini vilevile na Mazingira ya eneo hili ni kwamba unakuta kwamba kuna unyanyasaji ambao unafanywa na akina Baba dhidi ya akina Mama ambao pia kwa sasa ni kwa kiasi kidogo sana baada ya elimu kubwa kutolewa lakini kuna huu ukatili unaofanyiwa Watoto wa kike, “-Afisa Mtendaji Kata ya Kasamwa.
Eliud Mtalemwa ni Meneja Mradi KAGS kutoka Shirika la Rafiki SGO amesema lengo la Mradi ni kuhakikisha watoto wakike wanabakia shuleni kuanzia miaka 9 mpaka 15 kwa hiyo tunafahamu kwamba kuna changamoto mbalimbali katika Jamii yetu ambayo kwa namna moja ama nyingine zinarudisha jitihada za mtoto wa kike kubaki Shuleni.
Eliud ameendelea kwa kusema toka wameanzisha mradi huo matokeo yake yamekuwa ni makubwa kutokana na wanajamii kupata uwelewa kuzidi kuongezeka juu ya athari ya kuongezeka kwa Matukio ya ukatili wa kijinsia lakini pia na umuhimu wa kumwezesha mtoto wa kike kusoma.
“Kwa Mfano tumeshuhudia Ongezeko la matukio ambayo yanaibuliwa kwenye Jamii kwasababu zamani wanajamii hawakuwa na uwelewa wa namna ipi sasa waweze kutoa taarifa wanaposhuhudia vitendo vya ukatili wa kijinsia lakini kupitia mashindano haya wanajamii wanaweza kupata ujumbe wana namna ipi ya kupata ujumbe kwa hiyo tumeona vitendo vingi vinaibuliwa vya Ukatili wa kijinsia , “-Meneja Mradi KAGS.