Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Kigoma imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi Million 67,468,800 katika kipindi cha mwezi January hadi March 2020.
Akizungumza na Waandishi wa habari April 17 2020 Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Kigoma Nestory Gatahwa amesema fedha hizo zimeokolewa kutokana na operesheni mbalimbali za uchunguzi zilizohusisha Chama cha Ushirika cha RUMAKO kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Chuo cha Uganga Maweni pamoja na Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo.
KAMANDA ASIMULIA MAJAMBAZI SABA WALIVYOUAWA, MAPAMBANO MAKALI YA KURUSHIANA RISASI