Mwanzoni mwa wiki hii kuna taarifa zilienea katika mitandao ya kijamii kwamba gari la Mgombea ubunge kupitia chadema Musoma Vicent Nyerere lilikutwa na milipuko wakati akifanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyabisale Kata ya Bweli Musoma Mjini, leo Kamishina Msaidizi na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Philip Alex Kalangi amezungumza na ripota wa millardayo.com kuhusu ukweli wa taarifa hiyo.
‘Kuna watu wawili ambao wanafahamika kwa majina ya Goodluck Msuya miaka (42) Dereva wa Mgombea Ubunge Musoma Mjini pamoja na Salum Blein ambae pia ni mlinzi wa mgombea Vicent Nyerere wamekamatwa wakiwa na milipuko kumi na tano aina ya Explogel 7M V6 Watergel explosive’- RPC Philip Kalangi
‘Milipuko hiyo ilikutwa kwenye gari la Mgombea Ubunge lililokuwa likiendeshwa na dereva wake kabla ya kukamatwa watu hawa, Mgombea Ubunge Ndugu Vicent Nyerere alikuwa akiendelea na mkutano ndipo mlinzi wake alikwenda jukwaani na kumpa taarifa kwamba ndani ya gari lake kuna milipuko, mgombea huyo wa ubunge aliwambia wavipeleke vitu hivyo jukwaani na ndugu Nyerere aliwatangazia wananchi kuwa kuna watu wanataka kumuuwa na wamemtegea bomu ndani ya gari lake’ – RPC Kalangi
‘Katika uchunguzi wa awali wataalamu wa uchunguzi wamesema kweli ilikuwa ni milipuko ambayo kwa wakati huo ilikuwa haijafikia wakati ya kuleta madhara na kutokana na maelezo ya awali dereva na mlinzi wa Mbunge huyo yalitia shaka na ndipo ilipelekea kukamatwa kwani muda wote wao ndio walikuwa na gari hilo na hakuna mtu mwingine alilitumia kwa siku hiyo, kwa sababu sio swala la kawaida tukishagundua kuwa ni mifuko na ukaweza kubeba na kuurudisha’-RPC Kalangi
‘Kuhusu kwamba walikuwa wametega bomu la kutaka kuumua Mheshimiwa hilo bado tunalichunguza kutokana na mazingira ya tukio lenyewe lilivyotokea na tayari mgombea Ubunge ameshahojiwa ametoa maelezo yake bado tunaendelea kuhoji watu wengine’-RPC Kalangi
Unaweza ukabonyeza Play kumsikiliza RPC wa Mara Philip Kalangi
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE