Mtangazaji wa Clouds Fm Millard Ayo pamoja na Nakaaya Sumari mkurugenzi wa kampuni ya kaikaya, wamekutana na watu wa Arusha kwa lengo lakubadilishana mawazo na uzoefu wa kibiashara hasa kujikita zaidi katika mitandao ya kijamii.
“Moja ya mbinu ambayo ni nzuri kwenye maisha ya kila siku ni lazima utoke ukutane na watu,ukiwa mtu wa kujifungia unajifungia milango mingi ya kibiashara na kifedha pia pamoja na kwamba tunatakiwa tutumie nguvu kubwa kutangaza bidhaa zetu kwenye social media tuhakikishe bidhaa zetu ni bora kingine tusiogope kutangaza kwenye social media”-Millard Ayo