Katika kuendelea kupambana na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI nchini nazo Taasisi za Serikali kwa kushirikiana na Taasisi binafsi zimeendelea kutoa elimu ya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Wilayani Chato Mkoani Geita.
Pudenciana Mbwiliza Mwenyekiti wa Mtandao wanaoishi na Virusi vya UKIMWI nchini Tanzania akiwa mkoani Geita wilayani Chato katika wiki ya vijana ambapo kitaifa imezinduliwa na Waziri Mkuu wa Tanzania amesema lengo la ujio wao ni kuja kutoa elimu inayolenga namna ya kujikinga na Virus vya UKIMWI kwa makundi mbalimbali hasa kundi la vijana likionekana kupewa kipaumbele.
”Lengo letu ni kuifikia Jamii husika kama baraza katika kutoa elimu hii na ndio maan katika wiki ya vijana hapa Mkoani Geita wilayani Chato tumeanza na wanafunzi ,watu wazima lakini pia tunatoa elimu hii katika jamii ili kupunguza maambukizi kwa vijana, “Mbwiliza.
Amesema tumepanga kuifikia jamii kutokana na Maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kushamili kwa kiasi kikubwa hasa kwa upande wa vijana kwani ndio Taifa la kesho pia amewataka vijana kuendelea kujitokeza kupima afya na kupewa ushauri nasaa.
“Mimi mwenyewe naishi na Virus vya UKIMWI na nina mchumba angu pia anaishi na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI MUNGU akijaalia basi tutakuwa na familia yenye watoto kwa hiyo nawahimiza watu wasiogope kuja kupima na kupata ushauri, “ Mbwiliza.
Nao Baadhi ya wanafunzi kutoka shule ya Sekondari Chato waliokuwa wakipatiwa elimu hiyo wamesema kwa kiasi kikubwa wameongeza wigo mpana katika masuala mbalimbali juu ya Maambukizi ya virus vya UKIMWI huku wakitaka elimu hiyo kutolewa katika maeneo mbalimbali yanayoizunguka jamii.
“Nimejifunza vitu vingi jinsi ya kujikinga lakini elimu hii pia nitaipeleka kwa wanafunzi wenzangu nambao hawajapata nafasi katika kupata elimu hii naomba hata hii elimu ya ukimwi itolewe mashuleni nafikiri vijana watajua na kutambua mambo mhimu yahusuyo Ukimwi,” Mwanafunzi.