Ikiwa baadhi ya Ligi zimemalizika na nyingine zikielekea ukingoni kumalizika headlines na presha imeanza kuwa kubwa kwa mashabiki ya kutaka kufahamu ni wachezaji gani wataitwa kuzichezea timu zao za taifa, Argentina tayari wametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 35 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Presha ikiendelea kutawala kuhusiana wachezaji gani tutawaona Wolrd Cup 2018, staa wa club ya Real Madrid anayeichezea club ya Sporting Lisbon ya kwao Ureno kwa mkopo Fabio Coentrao amewashangaza wengi baada ya kuamua kutangaza kuwa asijumuishwe kwenye kikosi cha Ureno kitakachocheza Kombe la Dunia.
Fabio Coentrao ametangaza kuwa hajastaafu kuichezea timu ya taifa na ataendelea kuichezea lakini angeombwa asiitwe kwenye kikosi cha Kombe la dunia kwa ajili ya kupumzika kutokana na kutumika sana katika club msimu huu.
Fabio Coentrao mwenye umri wa miaka 30 kwa sasa ameombwa asiitwe kutokana na kuchoka kupita kiasi kutokana na kuitumika sana na club ya Sporting msimu huu “Baada ya majadiliano na timu ya taifa wiki iliyopita nimewaambia viongozi wa timu ya taifa kwamba baada ya msimu kuchoka sana najiona sipo katika hali nzuri ya kuichezea timu ya taifa lakini nitapatika kwa mechi zijazo”
Aliyoyasema Samatta ameyatimiza, tutamuona Europa League 2018/19?