Nchini Misri, ongezeko la watu liko chini zaidi kwani mnamo 2023, ilipungua hadi 1.4%, kiwango chake cha chini zaidi katika miongo kadhaa, kulingana na takwimu za Wizara ya Mipango iliyochapishwa Alhamisi.
Misri ndiyo nchi yenye watu wengi zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu, ikiwa na wakazi milioni 106, kulingana na wakala rasmi wa takwimu wa Misri.
Kushuka kwa idadi ya watu ni habari njema kwa serikali.
Rais Abdel Fattah al-Sisi alikuwa tayari ameonya juu ya mzigo wa kiwango cha kuzaliwa kwa fedha za umma na huduma za serikali.
Wakati ambapo 60% ya watu wanaishi au karibu na mstari wa umaskini. Si hivyo tu, bali nchi pia inakabiliwa na upungufu wa miundombinu kwa upande wa shule na hospitali, miongoni mwa mambo mengine. Na inaporomoka chini ya uzito wa deni linalokua.
Ili kupunguza msukumo wa idadi ya watu, viongozi walizindua kampeni ya 2019, “Deux, c’est assez” (wawili inatosha)