Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Vijana wasioona washairi nilipowatembelea Buigiri. Tupendane. Chuki humtafuna zaidi mwenye nayo #JumaaKareem pic.twitter.com/XVhGpK1iCq
— January Makamba (@JMakamba) January 23, 2015
#RaisMpya anatakiwa radical: aimarishe shule za sekondar kwa kupunguza idadi yake, na zile zinazopunguzwa ziwe VETA. Huu ni uamuzi wa haraka — Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) January 23, 2015
#RaisMpya anatakiwa awe pragmatic: aongeze ajira kwa kujenga viwanda vyenye backward linkage na kilimo. Kwa wingi. Value chain ikamilike!
— Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) January 23, 2015
Ushauri kwa Mhe bingwa wa uongo uliyeiba mali ya umma…huwezi kusafishika kwa kutunga na kusambaza uongo dhidi ya wanaosema ukweli juu yako — Reginald Mengi (@regmengi) January 23, 2015
SO READY!!…this 14th feb releasing my new song with GELLY !special for valentines!!Beautiful melodies with sexxy words
— PAPPINATION (@hemedyPHD) January 23, 2015
Facebook
CloudsFM
1. Radi yaleta maafa kijiji cha Bulembo kamachumu, Bukoba ambapo radi hiyo iliyoambatana na mvua kubwa imeua ng’ombe zaidi ya ishirini.
Blog
Mwananchi: Ukawa kuhamasisha wananchi wasipige kura ya maoni Katiba mpya
Dar es Salaam. Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimetangaza rasmi kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni ya katiba na kwamba kuanzia sasa vitahamasisha wananchi kuunga mkono.
Uamuzi huo umetolewa leo na wenyeviti wa vyama wanaounda umoja huo wa ukawa ambao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD, Makaidi.
Akizungumza wakati wa kutoa msimamo huo Profesa Lipumba amesema wamefikia uamuzi wa kutoshiriki katika zoezi hilo kwa sababu mchakato mzima haukuwa na maridhiano ya kitaifa.
“Vyama vya siasa ikiwemo CCM vilikubaliana mwaka jana kwamba zoezi la kura za maoni lifanyike mwaka 2016 baada ya uchaguzi mkuu, tulisaini wote na Rais Jakaya Kikwete alikubali, kwa nini mabadiliko yafanyike ghafla” amehoji Profesa Lipumba.
Amesema jambo la kushangaza, Rais Kikwete aligeuka na kutangaza kwamba Aprili 30, mwaka huu kuwa siku ya kupiga kura ya maoni kuhusu Katiba Mpya.
Amesema pamoja na kutangaza siku ya kupiga kura, bado uandikishaji katika daftari la wapiga kura haujaanza kwa sababu wanasubiri vifaa.
“Hadi sasa vifaa vya Biometric Voter Registration (BVR) vilivyopo ni seti 250 wakati vinavyohitajika ni seti 7500, tume inasubiri hadi sasa, zoezi hili litafanyika kweli?,” alihoji Lipumba.
“Mbinu hiyo inafanywa na Serikali kwa sababu Wazanzibari ndiyo wanaona kikwazo kwao,” alisema Makaidi.
Aprili 16 mwaka jana, Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kutoka vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD walitoka nje wakidai bunge hilo lilikuwa halijadili maoni ya wananchi yaliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Flora Mtegoa: Nitaendeleza ndoto za Kanumba (Mama Mzazi wa Marehemu Kanumba)
Mama wa aliyekuwa nyota wa filamu nchini, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema kuwa kupitia Kampuni ya Kanumba The Great Film inakamilisha uanzishaji wa taasisi itakayoitwa, Kanumba Foundation.
Pia, alikanusha uvumi kuwa kampuni ya Kanumba imekufa, akifafanua jambo hilo alisema kampuni hiyo inaendelea na shughuli zake. Alisema kutakuwapo Kanumba Foundation ili kusaidia jamii wakiwamo wasanii katika masuala mbalimbali.
BBC Arsene Wenger:”Vibali vya kazi vifutwe”
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ametaka kanuni za kutoa kibali cha kufanya kazi kwa ajili ya wachezaji ambao hawamo kwenye umoja wa ulaya zifutwe.
Wenger anaejaribu kumsajili Gabriel Paulista kutoka Villarreal ambae anahitaji kibali cha uidhinisho toka nchini kwake sababu hajawahi kulitumikia taifa lake.
Bosi huyo amekosoa mpango wa mapendekezo ya kupunguza idadi ya wachezaji toka mashirikisho yasiyo ya Umoja wa Ulaya wenye pasipoti katika michezo ya ligi ya England msimu ujao.
Akasema “Kusema ukweli inapaswa funguliwa kabisa, na kila mtu anaweza kungia”
Kwasasa kibali cha kufanyia kazi kwa nchi zisizo umoja wa Ulaya kunahitajika kuwa katika nafasi 70 za juu katika ubora wa viwango vya Fifa na awe amecheza kwa asilimia 75 katika timu ya taifa ndani ya miaka miwili.
“Ili kumsajili Paulista tungeweza kuwashawishi maofisa wa kwao kuwa ni beki wa kipekee mwenye kipaji.”
Chama cha Soka cha Englan kinataka kupunguza idadi ya wachezaji wasiokua wenyeji wa jumuiya ya ulaya kufikia asilimia 50 kwenye ligi.
Lakini Wenger anadhani kuondoa kanuni itakuwa bora kwa ajili vijana wachezaji Kiingereza.
“kufunga mipaka ya nchi na kuruhusu kucheza wachezaji wa Kiingereza tu Nini kitatokea? Ni kuua mvuto wa ligi dunia kote.
Wenger alisema Arsenal walitaka kumsajili winga wa kimataifa wa Ajentina Angel Di Maria lakini kibali cha kazi kikaleta shida.
Wenger aliongeza “Tulimtambua Di Maria alipokuwa 17.Tulimuona akiwa katika mashindano ya kimataifa na tulitaka aje hapa.
“Lakini alikwenda Ureno, na kutoka Ureno alikwenda Hispania. Kwa nini? Kwa sababu hakuweza kupata kibali cha kufanya kazi England.
Saleh Jembe
TFF MAPEMAA YAIONYA YANGA SUALA LA KUGOMA
Saa zaidi ya 24 baada ya Yanga kutishia kugomea kuingiza timu uwanjani, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema endapo klabu hiyo itathubutu kufanya hivyo, basi itakutana na rungu la sheria kali za Ligi Kuu Bara.
Yanga ilitoa tamko hilo, ikishinikisha TFF iwachukulie hatua kali waamuzi wa mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting, wachezaji wa Ruvu waliomchezea ‘kibabe’ straika wao, Amissi Tambwe.
Selestine Mwesigwa ambaye ni Katibu wa TFF, ameliambia gazeti hili kuwa, wao wanasubiri taarifa ya maandishi na hawawezi kufanya kazi kwa shinikizo.
“Kuhusu suala la kugoma, nafikiri Yanga wanaelewa kila kitu kuhusu sheria, kanuni na taratibu za ligi, kama kuna malalamiko, wao wanajua waende wapi.
“Kuhusu kutoa maamuzi ya mchezo wa Yanga na Ruvu, hatuwezi kuzungumza lolote kwa kuwa hatujapata ripoti husika ya mchezo.
“Kuhusu ripoti ya kamishaa kuwekwa wazi hilo halitawezekana kwa kuwa hiyo siyo taratibu, kama hii ikiwekwa wazi ina maana basi kila ripoti itabidi iwekwe wazi,” alisema Mwesigwa.
Tambwe alikutana na shuruba hiyo katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa ambapo alikuwa na wakati mgumu katika kumpita beki wa Ruvu, George Mich
JULIO APATA PIGO, MDOGO WAKE AUWAWA NCHINI AFRIKA KUSINI
Kiungo wa zamani wa Malindi ya Zanzibar, Shaku Kihwelo amefariki dunia baada ya kumwagiwa maji na mtu mmoja aliyetambulika kuwa ni raia wa Zimbabwe.
Kiungo huyo ambaye ni mdogo wa Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo amefariki dunia nchini Afrika Kusini na tayari tayaribu za kuleta mwili wake nchini kwa ajili ya mazishi zimeanza.
Kaka yake mwingine, Mwanamtwa Kihwelo amethibitisha kuhusiana na kifo cha mdogo wake huyo aliyewahi pia kuichezea Twiga FC.
“Kweli alimwagiwa maji na huyo Mzimbabwe ambaye walipishana kauli. Aliungana sana tumboni, juhudi za madaktari hazikuweza kuzaa matunda na ndiyo tumekutana na matatizo hayo.
“Tunatakiwa takribani randi 18,000 ili kuhakikisha mwili unafika nyumbani kwa ajili ya mazishi,” alisema Mwanamtwa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook