Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Nashukuru sana sana kwa salamu nyingi za upendo na za kutia moyo za siku ya kuzaliwa. Mungu atubariki sote.
— January Makamba (@JMakamba) January 29, 2015
Usimhukumu mtu kwa jambo la kusikia, na hata ukasikia jambo, hakikisha kwanza kama ni kweli limetendwa. — Izzo_bizness (@Izzo_bizness) January 29, 2015
Viongozi wetu mnatuangusha sana,pigieni kelele basi na vitu kama hivi vibadilike siyo kila siku madini tu.
— Flaviana Matata (@FlavianaMatata) January 29, 2015
Ndoto yangu ni tz kumiliki rasilimali zake na kuondoa umaskini wa watu wake..niambie ndoto yako juu ya Tanzania
— Nick Mweusi (@nikkwapili) January 29, 2015
Blog
BBC: Msafara wa rais Goodluck wapigwa mawe
Msafara wa magari ya Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan umepigwa kwa mawe na watu wanaioishutumu serikali kwa kukosa kukomesha harakati za wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.
Madirisha ya magari kadhaa kwenye msafara huo yalivunjwa kwa mawe, kabla ya polisi kuwafyatulia gesi ya kutoa machozi watau hao huku wakiwacharaza kwa mijeledi.
Shambulizi hili limefanyika katika mji wa Yola Mashariki mwa Nigeria, ambako Rais Jonathan alikuwa anaendesha kampeni yake kabla ya uchaguzi mkuu mwezi ujao.
Maelfu ya wakimbizi wa ndani wanaishi mjini Yola baada ya kutoroka vita kutoka makwao ambako Boko Haram inaendesha harakati zake.
Chelsea kumuuza mchezaji Schurrle
Chelsea imekubali kumuuza mshambuliaji wake Andre Schurrle ili kupata ufadhili wa kumsajili Juan Cuadrado.
Hatua hiyo ya kumsajili Cuadrado mwenye umri wa miaka 26 inaweza kukamilishwa katika mda unaohitajika kwa yeye kuichezea Chelsea dhidi ya Mancity siku ya jumamosi.
Gazeti la Mail online limegundua kwamba makubaliano hayo ambapo takriban pauni millioni 60 zitatumika yanakaribia katika kipindi cha saa 24 zijazo.
Chelsea inamuuza Shurrle kwa kitita cha pauni millioni 30 huku kilabu ya Wolfburg ikimhitaji nayo Borussia Dortmund pia nayo ikimtaka.
Kocha Jose Mourinho hampendelei mchezaji huyo wa Ujerumani,lakini anatambua thamani yake katika soko la uhamisho.
Mshambuliaji huyo wa Ujerumani vilevile anataka kurudi nyumbani.
Arsenal yamsajili Paulista
Klabu ya Arsenal nchini Uingereza imemsajili beki Gabriel Paulista kwa kitita cha Yuro millioni 15 huku mshambuliaji wa Arsenal Joel Campbell akijiunga na kilabu ya Villareal kwa mkopo hadi msimu wa joto.
Mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 24 alishiriki kila mechi ya Villa Real na huenda akacheza mechi yake ya kwanza katika uwanja wa Emirates dhidi ya Aston Villa siku ya jumapili.
Paulista ameweka sahihi kandarasi ya miaka minne na nusu katika uwanja wa Emirates na atalipwa mshahara wa pauni 60,000 kwa wiki.
Hivi Sasa.co.tz
Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, hali sio shwari katika kijiji cha Sisi kwa Sisi tarafa ya Mlingotini kufuatia mvua kuezua nyumba 51 za makazi ya wananchi. Mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali imeharibu zaidi ya nyumba 51, ambapo Wananchi wa kaya zaidi ya 25 wakosa kabisa sehemu ya kuishi.
Father Kidevu
Wanachama 30 wa Chama cha Wananchi CUF, leo wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na kusomewa mashitaka matatu yanayo wakibili.
Washitakiwa hao waliofikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Emmilius Mchauru wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu walisomewa mashitako hayo matatu ambayo ni Kula njama ya kufanya jinai kesi inayowakabili watuhumuwa wote 30 kosa walilolitenda huko Temeke.
Kosa la pili ni kufanya mkusanyiko usio halali na kosa la tatu ni kufanya mgomo wa katazo halali la Jeshi la Polisi ambapo kosa la pili na tatu linawakabili mtuhumiwa wa kwanza hadi 28.
Masharti ya dhamana yalikuwa wazi kwa watuhumiwa hao.
Saleh Jembe:
TFF YAWATAHADHARISHA WAZANZIBAR NA MIGOGORO KWENDA KORTINI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)l imepokea kwa masikitiko taarifa za kuwepo tena kortini kwa kesi dhidi ya uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), jambo ambalo linaweza kuathiri ushiriki wa timu za Zanzibar kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, na Kombe la Shirikisho.
Mwishoni mwa mwaka jana, TFF ilihadharisha juu ya masuala ya mpira wa miguu kupelekwa mahakamani, kwani kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za uendeshaji mpira wa miguu ambazo zinakataza masuala ya mchezo huo kupelekwa katika mahakama za kawaida.
Kutokana na hali hiyo, TFF iliiandikia barua ZFA kutaka mgogoro huo uondolewe kortini na yenyewe kuridhia kuwa tayari kupeleka ujumbe Zanzibar ili ukutane na pande zinazohusika.
Pia TFF ilisema timu za Tanzania Bara zisingeruhusiwa kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 iwapo kesi hiyo ingeendelea kuwepo kortini na kutaka iondolewe bila masharti yoyote.
ZFA iliithibitishia TFF kuwa kesi hiyo imeondolewa kortini bila masharti, hivyo timu za Tanzania Bara kuruhusiwa kushiriki katika michuano ya Kombe la Mapinduzi. Ni muhimu suala hilo likashughulikiwa haraka ili kutohatarisha ushiriki wa timu za KMKM na Polisi kwenye michuano hiyo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
FIFA WATUA NCHINI KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UPANGAJI MATOKEO
Ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) upo nchini kuchunguza tuhuma za upangaji matokeo.
Waamuzi waliosimamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na watu wengine watahojiwa na ujumbe huo. Matokeo ya uchunguzi huo yatatangazwa na Fifa baada ya shughuli hiyo kukamilika.
Tunaendelea kuwahimiza wanafamilia wa mpira wa miguu wazidi kuzingatia kanuni za maadili za TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) na Fifa katika utendaji wao. FIFA itahakikisha kuwa haki inatendeka katika uchunguzi ambao inaufanya.
Mwananchi:
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema angependa kuona sheria inayataja makosa ya udokozi bandarini kama ya uhujumu wa uchumi ili watuhumiwa wanapokamatwa na kushtakiwa wasipewa dhamana.
Waziri Sitta alisema hayo jana wakati akizungumza na watendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), katika mfululizo wa ziara zake kwa mashirika, taasisi na mamlaka zilizo chini ya wizara yake kwa lengo la kufahamiana na kujua changamoto na kupanga mikakati yake katika utendaji.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook