Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
#WizarayaNishatinaMadini imedanganya #Bungeni leo kuwa hakuna #MgomoMafuta , ukweli ni kwamba kuna #MgomoBaridi unaendelea #Dsm
— MNYIKA John John (@jjmnyika) June 29, 2015
Wananchi wa Irugwa wataja kero zinazowakabili, Usafiri na Umeme. Kinana azungumza na N/Waziri wa Nishati na kuahidi kuleta mtambo wa Umeme. — Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) June 29, 2015
Clouds FM
Uchaguzi wa Ubunge umendelea nchini Burundi licha ya wiki ya maandamano ya ghasia dhidi ya uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kutaka kuwania muhula wa tatu.
Zaidi ya watu 70 wameuawa tangu mgogoro huo uanze.Karibu watu 130,000 wamelitoroka taifa hilo. #Pichani: Ni Rais Pierre Nkurunziza alipokuwa akiwasili katika kituo cha kupigia kura huko Ngozi, Burundi
Blog
HIVISASA.CO.TZ
Serikali imetoa onyo kali kufutia kuwepo taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kwamba kutakuwepo na mgomo wa wauza mafuta nchini Tanzania suala litakalopekea kuwepo uhaba wa mafuta ya Petrol na Dizeli nchini Tanzania.
Akizungumza Bungeni mijini Dodoma asubuhi hii Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage amesema kwamba serikali itawachukulia hatua wamiliki wa makampuni mafuta pale watakapo kiuka na kuvunja sheria ikiwemo kufanya mgomo hali ya kuwa mafuta yapo.
Mwijage amesema ameona kwenye mitandao ya kijamii taarifa kwamba katika siku mbili zijazo nchi inaweza kukosa mafuta katika vituo mbalimbali nchini kutokana na tishio la mgomo huo.
Amesema kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini anawahakikisha wananchi kwamba haiwezi kutokea mgomo wa mafuta nchini, kwa sababu wanajua kwa takwimu katika hifadhi za Dar es salaam zinaonesha kuwa kuna mafuta ya kutosha.
Amesisitiza kuwa Sheria na kanuni zinampa mamlaka Waziri kuruhusu mafuta yauzwe, pia sheria za EWURA zinaweza kumfungia mtu yeyote mwenye mafuta anayekataa kuyauza
Kwa upande mwingine amewataka wenye vituo kuruhusu mafuta yauzwe na kusisitiza kuwa asitokee mtu yeyote kufanya uvumi huo kuwa ukweli.
Urais 2015: Watia Nia CCM Wafikia 42
Mwanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) Banda Sonoko (46) amechukua fomu ya kuomba raidhaa ya kuteuliwa ndani ya chama cha Mapinduzi kugombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba 2015.
Mgombea huyo anakuwa wa 42 kuchukua fomu huku akitakiwa kurejesha fomu hizo siku ya ijumaa ambapo yeye na wagombea wengine wanatakiwa wawe wamewasilisha vielelezo vyao ikiwamo majina ya wadhamini 450 kutoka mikoa 15, kati ya hiyo mitatu ya Zanzibar.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu jana Sonoko amesema kaulimbiu yake ni kutokomeza umaskini na kwamba anaamini katika usimamizi jambo hilo endapo atafanikiwa kuwa rais.
Ameongeza kuwa ameamua kufanya hivyo kwa sababu anazo sifa, vigezo na uwezo kwamba ndiye anayeweza kuvaa viatu vya Mwalimu Julius Nyerere.
“ CCM imefanya mambo makubwa katika uongozi wake ikiwamo kutengeneza miundombinu ya kutosha na sasa kinachotakiwa kuisawazisha… “Miji yetu imeshakaa vizuri sasa nchi yetu inahitaji greda liweze kusawazisha… na greda ni mimi, nitaweza kusawazisha matatizo yaliyobaki na kuweza kuhakikisha lindi la umaskini linaondolewa.”amesema Banda Sonoko.
Mwanaspoti
TRAIKA, Hamis Kiiza, ambaye ni raia wa Uganda amefunguka kwamba atawasili Dar es Salaam wiki hii na ataichezea Simba msimu ujao wa Ligi Kuu Bara akisisitiza kuwa atacheka na nyavu kama atakavyo kwani yupo kwenye ubora wake wa juu.
Kiiza mchezaji wa zamani wa Yanga, alikiri kuwa ni kweli Mbeya City walimtaka, lakini klabu hiyo si ya hadhi yake.
Kiiza alifunguka kila kitu baada ya kuulizwa atakuwa wapi msimu ujao, ndipo akatamka anaenda Simba. “Tumeshakubaliana na Simba na nitaenda Tanzania kukamilisha baadhi ya mambo,”alisema Kiiza.
Alipoulizwa kuhusu Mbeya City, Kiiza alisema: “Ni kweli Mbeya City walinitaka, lakini kusema kweli kwa sasa bado siyo hadhi yangu. Ninachokwambia, naenda Tanzania wiki ijayo na nitacheza ligi ya Tanzania msimu ujao,” alisema alipozungumza na Mwanaspoti wikiendi.
Tambwe ang’aka pengo la Ngasa
TRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe amesema kiwango kilichoonyeshwa na Deus Kaseke na Geofrey Mwashuiya katika mechi mbili za kirafiki walizocheza kimethibitisha kuwa pengo la mshambuliaji aliyeondoka klabuni hapo, Mrisho Ngassa halitakuwepo.
Ngassa ametimkia nchini Afrika Kusini alikokwenda kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Free States hivyo kuacha taharuki juu ya pengo lake katika kikosi hicho.
Tambwe alisema nyota hao wawili wapya wana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kasi na kupiga pasi za maana jambo ambalo limeifanya Yanga kuwa hatari zaidi.
“Hakuna pengo la Ngassa pale, vijana wamecheza vizuri sana katika mechi hizi mbili, tunahitaji kuzoeana tu zaidi ili tufanye makubwa,” alisema Tambwe aliyeifungia Yanga mabao 16 mashindano yote msimu uliopita.
Yanga imecheza mechi mbili za kirafiki wiki iliyopita ambapo iliifunga Friends Rangers mabao 3-2 kabla ya kutoka sare tasa na Villa SC ya Uganda.
Saleh Jembe
SOMA HAPA UJUE NDOA YA OKWI ILIVYOTIKISA UGANDA
NDOA ya mchezaji wa Simba, Emmanuel Okwi, raia wa Uganda, aliyofunga na Nakalega Florence, juzi Jumamosi kwenye Kanisa la Lubaga Miracle Center, linaloongozwa na Mchungaji Robert Kayanja, ilionekana kutikisa viunga mbalimbali vya Jiji la Kampala nchini hapa.
Kutikisa kwa ndoa hiyo kulitokana na vyombo mbalimbali vya habari kuitangaza ndoa hiyo mara kwa mara hasa siku yenyewe ya tukio.
Utaratibu wa ibada ya ndoa hiyo ulianza saa saba kamili mchana ambapo waumini na watu wote waliofika kanisani walisachiwa wao na vitu walivyobeba kwa kutumia kifaa maalum na kisha kupitishwa sehemu nyingine ya kuukagua mwili wote zoezi ambalo lilisimamiwa na askari polisi waliokuwa na silaha.
NIZAR, KADO WANUSURIKA KATIKA AJALI MABYA YA GARI MKOANI DODOMA
Kiungo wa zamani wa Yanga, Nizar Khalfan amenusurika na ajali mbaya ya gari iliyotokea eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
Imeelezwa, Nizar alikuwa pamoja na kipa mpya wa Mwadui FC, Shabani Kado ambaye ni kipa bora Tanzania Bara.
Hata hivyo, juhudi za kuwapata hazikufanikiwa baada ya mtoa habari kueleza wote wamenusurika katika ajali hiyo iliyohusisha gari aina ya Mitsubish walilokuwa wanalitumia.
Baadaye Nizar ambaye pia ametua Mwadui FC alitupia picha kwenye mtandao wa kijamii akieleza amenusurika.
“Tunamshukuru Mungu hadi sasa tuko salama,” alisema.
Taarifa zinaeleza wawili hao walikuwa safari kwenda Shinyanga kujiunga na timu yao mpya ya Mwadui FC kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
Majira.co.tz
LOWASSA: SILIPI KISASI, JK RAFIKI YANGU
WAZIRI Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, amesema maneno yanayosemwa kuwa akipata urais atalipiza kisasi ni ya uongo kwani Rais Jakaya Kikwete ni rafiki yake na Bagamoyo nyumbani kwake kwa pili.
Bw. Lowassa aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wana CCM waliojitokeza kumdhamini katika harakati za kusaka urais kupitia chama hicho kwenye Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani.
Aliongeza kuwa, Rais Kikwete ameongoza nchi kwa amani na kuifanya nchi iendelee kuwa tulivu pamoja na kulinda Muungano uliopo.
“Rais Kikwete amefanya kazi kubwa na mambo mengi hivyo anastahili kupewa medani na anahitajika kiongozi makini ambaye ataiendeleza miradi ambayo ataiacha,” alisema.
WALIMU WABAKWA, KUTESWA KISHIRIKINA
MBUNGE wa Mwibara, mkoani Mara, Bw. Kangi Lugola, amelazimika kukatisha vikao vya Bunge vinavyoendelea Mjini Dodoma na kwenda jimboni kwake, Kijiji cha Nambaza, Kata na Tarafa ya Nansimo, wilayani Bunda, ili kushughulikia adha wanayoipata walimu
wa shule ya msingi kijijini hapo.
Walimu hao wanadaiwa kufanyiwa vitendo vya kishirikina kwa kuteswa, kudhalilishwa hivyo kulazimika kuomba uhamisho ili wakafundishe shule nyingine zilizopo mbali na jimbo hilo.
Wakisimulia vitendo wanavyofanyiwa, walimu hao walisema usiku wakiwa wamelala, wachawi huwafuata na kuwanyoa nywele sehemu za siri, kuwaingilia kimwili, kuwaibia mali pamoja na fedha zao.
Walisema mbali ya vitendo hivyo, pia wamekuwa wakikuta mikojo, ugali na samaki ukiwa umefunikwa na shuka kitandani hali ambayo imewafanya washindwe kufundisha na kuomba wahamishwe.
Mwalimu Joyce Maugo ambaye ni mkongwe katika shule hiyo, alisema walimu wa shule hiyo wako hatarini kutokana na vitendo vya kishirikina wanavyofanyiwa ambapo mmoja wa walimu wa kike ambaye kimaumbile ni mdogo, aliingiliwa kishirikina hadi akazimia.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.