Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Karibu kusoma gazeti la leo la Mwananchi nimejibu maswali 10 ya wananchi ktk masuala mbalimbali yanayogusa jimbo langu la Ubungo
— MNYIKA John John (@jjmnyika) February 25, 2015
TANZIA: Aliyekuwa katibu wa Uvccm Wilaya ya Mtwara Vijijini Ndugu Seleman Said Libaki amefariki dunia jana jioni ktk hospitali ya Ligula.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) February 25, 2015
BBC
Shirika la kandanda duniani FIFA, limetangaza kuwa halitazilipa fidia klabu zozote za soka barani Ulaya ambazo hazijafurahia hatua ya FIFA kuandaa kombe la dunia nchini Qatar mwezi Novemba na Disemba ya mwaka wa 2022.
Katibu mkuu wa shirikisho hilo, Jerome Valcke, amesema kuwa FIFA haina haja ya msamaha wowote wa maandalizi ya uwenyeji wa mashindano hayo, ambayo yanatazamia kutatiza pakubwa ratiba ya michuano ya ligi kuu barani Ulaya.
Hapo jana mapendekezo ya jopo la FIFA yalisema kuwa mashindano ya kombe hilo la dunia nchini Qatar yatafanyika wakati wa baridi ili kuepuka msimu wa kiangazi katika mataifa ya ghuba ambayo hushuhudia joto kali mno.
Facebook #Fid Q
Mara yangu ya mwisho kufanya show na ‘ Live band ‘ Dar.. Ilikua ni kwenye Poetry Addiction ya kwanza kabisa, mnaonaje nikiu-upgrade huu uzinduzi wa kichupa cha #BongoHiphop utakaofanyika Jpili pale Billz kwa kuifanya show yangu na Live band pia!?
Hivisasa.co.tz
Watu 13 wamepoteza maisha kwa shambulio la kujitoa muhanga mjini Potiskum, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Mfanyakazi mmoja wa kituo cha basi cha Dan-Borno amesema kuwa aliyejitoa muhanga alisubiri mpaka basi hilo linalobeba Watu 18 kujaa kabla ya yeye kuingia kwenye basi hilo na hatimaye basi hilo kulipuka.
Shuhuda huyo amesema basi liliharibiwa vibaya na moto na mengine ya jirani kuharibiwa. Siku ya jumapili, mji huo ulishambuliwa na Msichana mmoja aliyejitoa muhanga.
Bongo 5.com
Mwanamuziki kutoka Nigeria Davido, ameweka wazi kuwa mwaka huu hatafanya collabo na msanii yeyote kutokana na kuwepo kwa maombi mengi tangu mwaka umeanza ya kumtaka kufanya collabo nao.
Akihojiwa meneja wa msanii huyo, Kamal Ajiboye, amesema kuwa kumekuwepo na maombi mengi kutoka kwa wanamuziki wakubwa na wadogo lakini msanii huyo ameyakataa kutokana na kuwekeza nguvu katika album ambayo anategemea kuitoa Julai mwaka huu.
Clouds.co.tz
Mwalimu Kibasila Sekondari aishi na kinyesi miaka miwili
Ama kweli dunia ina mambo, na ukistaajabu ya Mussa kweli utayaona ya Firauni kwa mwalimu huyu wa Sekondari ya Kibasila Jijini Dar Es salaam. Kwani katika hali isiyokuwa ya kawaida mwalimu Gaudensia Missanga mkazi wa Kisiwani kata ya Sandali wilayani Temeke anadaiwa kuishi katika chumba ambacho amehifadhi kinyesi hali ambayo inatishia usalama wa afya yake.
Hebu jenga picha, mwalimu wa shule ya Sekondari halafu anaishi ndani na kinyesi! Hivi hii imekaaje?
CLOUDS TV imeona isiishie tu kusikia juu ya tukio hilo, imefika hadi kwenye nyumba anayoishi mwalimu huyo anayefundisha masomo ya sayansi na kuzungumza na mwenye nyumba REUBEN SHAYO ambaye ameeleza kilicho sababisha kubaini uchafu huo.
‘’Tuliona funza wakitoka chini ya mlango wake na harufu mbaya ikitoka na mwenzetu hatujawahi kumuona akioga wala akiingia chooni ndiyo tukabaini hali hii,’’alisema Shayo.
Kwa upande wake mwalimu GAUDENSIA anayetuhumiwa kuishi na kinyesi kinachodhaniwa kuwa ni cha binadamu hakuweza kupatikana kujibu tuhuma hizo na alipopigiwa simu yake ya mkononi ilikuwa inaita bila majibu.
Hadi CLOUDS TV inaondoka nyumbani kwa mwalimu huyo chumba chake kilikuwa kimefungwa huku taratibu zingine zikiwa zinaendelea.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook