Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo na pia usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook twitter na instagram @millardayo ili niwe nakutumia kila kinachonifikia.
Kwenye zama za #HapaKaziTu, kila wakati inabidi kila mtanzania afikirie kuwa huu ni #WakatiWaKazi, basi na afanye… https://t.co/T2xqqOl0nu
— Hamisi Kigwangalla (@HKigwangalla) November 25, 2015
Mwananchi: Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda leo amewaweka ndani kwa saa sita maofisa ardhi zaidi ya 10 huko Kawe baada ya kuchelewa kufika eneo walilokubaliana kukutana.
Rweyunga blog
MLIPUKO ULIOLILENGA BASI LA WALINZI WA RAIS TUNISIA WAUWA WATU 12
Mlipuko umelilenga basi lililokuwa limebeba walinzi wa rais katika Jiji la Tunis nchini Tunisia na kuuwa watu 12.
Kufuatia tukio hilo rais Beji Caid Essebsi ametangaza siku 30 za hali ya hatari na kutangaza watu kutotembea ovyo katika Jiji la Tunis.
Tunisia imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya kundi la Dola ya Kiislam (IS), likiwemo tukio la mtu mwenye silaha kuwashambulia watu kwenye hoteli ya ufukweni ya Sousse mwezi Juni na kuuwa watu 38.
HABARI LEO
Muongozo elimu bure waandaliwa
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, amesema wizara yake inaandaa mwongozo utakaotoa maelekezo juu ya muundo, mfumo na utaratibu nyumbufu utakaohakikisha kuwa ifikapo Januari mwakani, elimu ya msingi inatolewa bila malipo.
Profesa Mchome alisisitiza juu ya utekelezaji wa kutoa elimu bure bila kuathiri ubora wa elimu itakayotolewa na kuziagiza taasisi zinazohusika pamoja na walimu kushughulikia kero zao katika ngazi mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa nyumba za walimu.
Alisema wizara yake inatarajia kuongeza uandikishwaji wa watoto wa awali kutoka asilimia 45 mwakani hadi asilimia 100 ifikapo mwaka 2020. Katika kikao hicho ambacho pia kilijadili mwelekeo wa Sera na Mipango ya Elimu katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano, Profesa Mchome alisema wizara inajipanga kuhuisha taratibu za kujiunga na taasisi zinazotoa elimu msingi na mafunzo katika ngazi mbalimbali.
Profesa Mchome alitoa vipaumbele elekezi 20 vya utekelezaji katika kuboresha sera na mipango ya elimu kwa kipindi cha miaka mitano kutoka 2015 hadi 2020. “Wizara ina mpango wa kuandaa mfumo, muundo na taratibu nyumbufu za kutoa elimu ya awali na elimu ya msingi bila malipo ili kuongeza uandikishwaji wa watoto wa awali kutoka asilimia 45 mwaka 2015 hadi asilimia 100 ifikapo mwaka 2020,” alisema Profesa Mchome.
‘Mazungumzo CUF, CCM hayazuii uchaguzi Z’bar’
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) – Zanzibar kimesema mazungumzo yanayoendelea nchini yakiwahusisha viongozi wakuu wa kisiasa kamwe hayajazuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu ambao matokeo yake yalifutwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).
Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa. Alisema hawawezi kukwepa mazungumzo katika kukuza demokrasia kama ni sehemu ya kuimarisha amani na utulivu wa nchi.
Hata hivyo, alisema mazingira hayo kamwe hayawezi kuwa mbadala wa sheria zilizopo nchini ambapo kwa upande wa ZEC imetangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu na kutaka wananchi wajiandae kutangaziwa tarehe mpya ya Uchaguzi Mkuu.
Alisema tayari Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imetangaza kufutwa kwa uchaguzi wa Oktoba 25 kupitia Gazeti la Serikali na hivyo kuashiria kutoa nafasi kwa ZEC kufanya maandalizi ya uchaguzi mwingine.
Mapema, Vuai aliwataka wana CCM Zanzibar kujiandaa na uchaguzi wa marudio na kuepukana na propaganda zinazotolewa na wapinzani kwamba hakuna uchaguzi mwingine. Alisema kwa upande wao wapo katika maandalizi ya uchaguzi mwingine ikiwemo kutayarisha mawakala watakaosimamia uchaguzi huo.
HIVI SASA.CO.TZ
BOT Yarejesha Chenji Za Sarafu
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imerejesha huduma ya chenji za sarafu ili kukidhi mahitaji ya chenji ya sarafu kwa wananchi pamoja na wafanyabiashara.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa huduma za Kibenki wa Benki kuu ya Tanzania (BOT), Martin Kobelo amesema hatua hiyo inafuatia kuadimika kwa sarafu ya shilingi 50, 100, 200,na 500 katika mzunguko wa fedha kwa watu na wafanyabiashara.
Amesema benki kuu imeanzisha dirisha la utoaji wa chenji za sarafu ambalo litaanza kufanya kazi kwa miezi sita ya mwanzo ili kuona kama uhitaji wa sarafu utaendelea kuwepo au utapungua.
Akizungumzia utaoaji chenji Kobelo amesema huduma hiyo ya chenji sasa itatolewa kikanda ambapo itatolewa na Benki kuu makao makuu na katika matawi yake ya Mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Zanzibar.
Kwa upande mwingine amesema kuwa huduma ya chenji ni bure kwa wananchi wote na hutolewa mara mbili kwa wiki, Jumanne na Alhamisi kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana.
DAR 24.COM
Aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba SC Selemani Matola, leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Geita Gold FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara.
Novemba 11 mwaka huu, Matola aliandika barua kwa ajili ya kuomba kujiuzulu ndani ya Simba kwa madai kuwa hana maelewano mazuri na kocha mkuu Dylan Kerr.
Matola amekuwa kocha msaidizi kwenye kikosi cha Simba kwa muda mrefu baada ya kuitumikia Simba kama mchezaji na nahodha pia
Geita Gold FC ipo kundi la C na inafanya vizuri kwenye kundi hilo ikiwa inachuana kwa karibu na JKT Oljoro FC inayoongoza kundi hilo ikiwa kileleni kwa pointi 14.
KIPINDUPINDU CHAPUNGUA DAR
Idadi ya wagonjwa wa kipindupindu jijini Dar es salaam imepungua kufikia wagonjwa kumi na mbili (12) kwa mkoa mzima, huku wilaya ya Temeke ikiwa na wagonjwa saba,Kinondoni wagonjwa wanne na Ilala ikiwa na mgonjwa mmoja
Haya yamezungumzwa na Mratibu wa Magonjwa ya kuambukiza wa Jiji la Dar es salaam Bw. Alex Mkamba ofisini kwake leo akielezea jinsi gani mkoa umefanikisha kupambana na kipindupindu kwa kuzingatia usafi katika jiji.
Ameongeza kuwa katika kufanikisha mapambano dhidi ya kipundupindu wametoa mafunzo juu ya mbinu shirikishi ya namna ya kujikinga na kipindupindu kwa watendaji wa mitaa na pia imewahimiza kukagua maeneo yao na kuwapa kibali cha kufunga maeneo ya biashara au maeneo yatoayo huduma za chakula yasiyozingatia usafi.
Akielezea kuhusu huduma kwa wagonjwa wa kipindupindu jijini Dar es salaam mratibu huyo amesema jiji lina dawa za kutosha za kuhudumia wagojwa ipasavyo kwa kuwapatia huduma bora zaidi kuendana na kasi ya maambukizi yaliyopo.
‘hata leo Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa dawa za kusafishia maji (Water Guard) maboksi 45 kwa kila wilaya’ – Mkamba
Aidha alisema serikali imejipanga katika kudhibiti maambukizi mapya kwa kuwapima wagonjwa kabla na baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini na aliwashauri wananchi kubadili tabia kwa kuhakikisha usafi unafanyika pia kuchemsha maji na kuufanya usafi kuwa ni tabia yao ya kila siku.
Mpaka sasa jumla ya watu 55 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu jijini Dar es salaam.(P.T)
Dewji blog
Serikali yatangaza kuacha kugharamia vikao kazi kwa watendaji wake, kuanza kutumia mfumo wa Video Conference
Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imetangaza kuacha kugharamia vikao vyote vya watendaji wa serikali na badala yake watakuwa wakitumia mfumo mpya wa mawasiliano wa video (video conference) kufanya vikao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Florence Temba katika ukumbi wa Habari Melezo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamko hilo la serikali kwa watumishi wake.
Temba amesema serikali haitahusika na gharama zozote za vikao vya watendaji wake na njia watakayokuwa wakitumia watendaji hao ni mfumo wa mawasiliano wa video conference ambao utawawezesha watendaji hao kufanya vikao sehemu yoyote walipo kwa kuwasiliana kwa njia ya picha na sauti.
Amesema kuwa njia hiyo ya kufanya vikao kwa njia ya video itawawezesha watendaji wao kupunguza gharama za matumizi ambazo zilikuwa zikitumika awali na hata muda ambao walikuwa wakiutumia awali kusafiri mikoani kwa ajili ya kushiriki vikao hivyo.
“Serikali haitaingia gharama mbalimbali ili kuendesha vikao kazi na watendaji wake na hatua hii ni matokeo ya serikali kuanza kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kutumia mfumo huu wa kisasa tunaweza kupunguza gharama kubwa ambazo zilikuwa zikitumika awali,” amesema Temba.
Temba amezitaja gharama ambazo serikali imezifuta kuwa ni pamoja na kukodi kumbi za mikutano, usafiri na muda ambao unatumika nje ya vikao vya kazi na walengwa ni makatibu tawala wa mikoa, maafisa wa utumishi na mamlaka za serikali za mitaa.
Aidha Temba amezitaka wizara, idara, wakala wa serikali na mamlaka za serikali za mitaa na watumishi wa umma kuhakikisha wanaboresha mawasiliano ya njia ya video ilikuweza kufanya vikao kwa njia hiyo na wanatakiwa kutembelea tovuti ya Ofisi ya Ris, Menejimenti ya Utumishi wa Umma www.utumishi.go.tz kwa ajili ya kupata mwongozo mahususi ili kufanikish kufanya vikao na watakuwa wakitumia huduma hiyo ya vido conference bure bila kutozwa gharama zozote.
Nae Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano (TEHAMA), Priscus Kiwango amesema mfumo huo wa vikao kwa njia ya mawasiliano upo tayari kufanya kazi kwani wamekuwa wakiutumia kufanya majaribio tangu mwaka 2013 na mpaka sasa wamefanikiwa kufanya vikao zaidi ya 10 kwa kutumia mfumo huo.
Kuhusu kukatika kwa mawasiliano, Kiwango amesema watakuwa wakitumia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika kufanikisha hilo na mkongo huo upo vizuri katika mawasiliano kutokana na kutokuwa ukiingiliana na mitandao mingine hivyo kufanya mawsiliano yao kuwa ya uhakika.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.