Leo July 13, 2018 kuna hii ya kuifahamu kumhusu Tajiri namba moja Afrika Aliko Dangote akihojiwa na gazeti la Financial Times amesema kwa sasa ana miaka 60 na yupo busy sana hawezi kutafuta mwanamke lakini akijitokeza wa kumuoa basi atafanya hivyo.
“Mimi si kijana nina miaka 60 sio mchezo na siwezi kutembea mtaani kutafuta mwanamke nakosa muda kabisa lakini akitokea wa kuwa naye sawa nitamuoa,“-Aliko Dangote.
Dangote amesema kuwa kwa siku anapigiwa simu zaidi ya mara 100 huku akipokea maelfu ya barua pepe.
Dangote mpaka hivi sasa ameachwa na wanawake wawili na amefanikiwa kupata watoto watatu ingawaje vyombo vya habari nchini Nigeria vinaripoti kuwa Bilionea huyo ameshawahi kuishi na wanawake watatu baada ya kuachana na wanawake wake wa ndoa lakini hajafanikiwa kuzaa nao.