Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema wapo baadhi ya watu ambao wanajipenyeza kupitia mgongo wa Taasisi za Dini nchini kujifanya Wahubiri kumbe ni wachochezi na wanajiingiza katika masuala ya kisiasa.
“Serikali ya Rais Dk. John Magufuli haitakua tayari kwa mwananchi yeyote kutumia mwavuli wa dini, au kufanya misikiti na makanisa kuwa kichaka kwa kufanya uchochezi katika nchi hii, kuhatarisha amani ya nchi hii, tupo makini na hatuwezi kuchezewa na mtu yeyote au taasisi yoyote,” Waziri Lugola
“Taasisi hizi za Makanisa na Misikiti wanao mchango kwa wananchi hususani waumini wao katika kuhubiri amani ya nchi hii, katika kukemea vitendo vya rushwa kwasababu hata katika maandiko rushwa imekemewe” Waziri Lugola
“Rushwa imeonekana ni hatari katika vitabu vyote vitakatifu vya dini, lakini wapo baadhi ya watu wasiowaaminifu nchini wamejipenyeza na wanaendelea kujipenyeza katika taasisi hizo, na badala ya kuhubiri masuala ya kiroho, wanajihusisha na masuala ya uchochezi na uvunjifu wa amani,” Waziri Lugola.
LIVE MAGAZETI: Kesi ya Rais, Lazima ulie, Sheikh atekwa, JPM kikao kizito na MA-RC