Leo November 29, 2018 Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company Dr. Freddy Msemwa ametangaza fursa mpya kwa Watu wanaohitaji kumiliki Nyumba wanazozijenga katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Dr. Msemwa amesema Mwananchi ambae amepangisha nyumba za WHC atapata fursa kwa kodi yake anayolipa mwisho wa mwezi hiyohiyo itatumika kununulia nyumba aliyopanga.
“Hivi karibuni Serikali imeridhia kuwauzia nyumba watu wa Sekta binafsi ikiwemo Viwanda, Benki, Makampuni ya simu, tunahakikisha nyumba tunazojenga zinaweza kununulika na Watu wa kawaida hasa wenye kipato cha kawaida” Dr. Msemwa
“Kipindi cha kulipia nyumba ni cha muda mrefu kwa maana kwamba mtu anweza lipa kwa mwaka mmoja au miaka 25 unavyopenda wewe, tunamuwezesha mtu kuanza kukaa akilipa kodi kama mpangaji lakini yeye mwisho wa siku kodi inahesabiwa katika malipo ya kununua nyumba” Dr. Msemwa
POLISI WALIVYOWADHIBITI WANACHAMA WA CHADEMA MAHAKAMA KUU, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA