Mkuu wa mkoa wa DSM Paul Makonda leo amekutana na mabenki, Wenyeviti wa mitaa, madalali wa mahakama na mabenki kuweka mkakati madhubuti wa kudhibiti wizi na utapeli ambao umekuwa chanzo cha maumivu kwa wananchi.
Katika kikao hicho RC Makonda amewataka watu wa Benki kuhakikisha wanafanya uchunguzi na kujiridhisha kabla ya kutoa mkopo baada ya kuibuka kwa utapeli wa watu kutumia hati za watu na kuchukuwa mkopo pasipo muhusika kujua jambo linalopelekea nyumba na mali za watu kupigwa mnada na kuacha familia zikikosa makazi.