Leo May 10, 2018 Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kutoka Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya ambapo walikuwa wanatumikia kifungo cha miezi 5.
Nje ya gereza Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akiongea na simu amesema wataendelea na taratibu za rufaa hata kama Sugu ameachiwa.