Rwanda imepiga marufuku usafiri wa umma na kibinafsi kati ya Wilaya na Mji Mkuu wa Kigali, uamuzi huo ni kutokana na hali ya kutisha ya maambukizi ya virusi vya corona.
Katika wiki moja tu Rwanda imerekodi Vifo vya watu 30 kutokana na ugonjwa huo, kulingana na kikao cha Baraza la Mawaziri hatua ya kupiga marufuku hiyo ya usafiri inaanza kutekelezwa leo Januari 5.
Hiyo ni moja wapo ya mikakati iliyochukuliwa kudhibiti wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.
Rwanda yenye watu Milioni 12 kwa mujibu wa takwimu za 2018 imesema hali imekuwa mbaya na ya kutisha kutokana na kuongezeka sana kwa visa vya maambukizi pamoja na vifo vya watu.
KAMATA KAMATA BIASHARA HARAMU WANAOHIFADHI WALEMAVU ILI WAKAOMBE MTAANI