Leo June 5, 2018 Mahakama ya wilaya ya Arumeru imeahirisha kesi inayomkabili Ofisa itifaki kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Arusha, Swalehe Mwindadi pamoja na mtumishi wa kitengo cha Masijala katika ofisi hiyo, Amina Mshana(29) hadi June 18 mwaka huu baada ya upelelezi kutokamilika.
Mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Sabina Silayo aliieleza jana mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo haujakamilika na kuomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Mara baada ya ombi hilo ndipo hakimu wa mahakama hiyo, Patricia Kisinda alihairisha hadi June 18 na kuamuru washtakiwa warejeshwe rumande.
Nje ya Mahakama Mama mzazi wa Lucas, amelalamikia jaribio la kutaka kurubuniwa kwa fedha kwa mtoto wake ili aachane na jambo hilo, hali aliosema hakubaliani nayo ukilinganisha na udhalilishaji aliofanyiwa mwanaye.
Watuhumiwa hao walifikishwa hivi karibuni katika mahakama ya wilaya ya Arumeru wakishtakiwa kwa makosa mawili ikiwemo kumvua nguo na kisha kumchukua picha akiwa uchi mwandishi wa habari wa kujitegemea mkoani Arusha, Lucas Myovela
Washtakiwa hao wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ambapo shtaka la kwanza ni kunyang”anya kwa kutumia silaha kinyume na kifungu cha 287A cha sheria ya kanuni ya adhabu kifungu kidogo cha 16 kilichorekebishwa mwaka 2002.