Aliyekuwa Rais wa Sudan Omar al- Bashir amefunguliwa kesi katika Mji Mkuu wa Taifa hilo Khartoum, akishtakiwa kwa Mapinduzi ya kijeshi yaliyomsaidia kuchukua madaraka zaidi ya miongo mitatu iliopita.
Bashir mwenye umri wa miaka 76 ambaye alihukumiwa kwa ufisadi, huenda akakabiliwa na hukumu ya kunyongwa iwapo atapatikana na hatia kuhusu jukumu lake katika mapinduzi hayo ya 1989.
Zaidi ya maafisa 20 wa zamani wanashtakiwa pamoja naye
Bashir alilazimishwa kuondoka madarakani mwaka 2019 kufuatia maandamano makubwa yaliyofanyika Sudan.