Rais John Magufuli amesema Serikali imekopa Shilingi Bilioni 520 za Mradi wa maji safi na maji taka unaotekelezwa JIjini Arusha na fedha hizo zitalipwa na Watanzania wote.
Amesema kama ilivyokuwa kwa mikopo mingine inavyolipwa na watu kutoka sehemu mbalimbali ndivyo hivyo itakuwa katika kulipa fedha hizo.
“Mradi wenu wa maji ni mkubwa sana, utazalishaji maji zaidi ya mara nne ya kiwango kinachohitajika Arusha, utagharimu BILIONI 520 fedha hizi ni mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika, Serikali tumekopa kwa ajili ya Arusha” -Rais Magufuli
“BILIONI 520 tumeziweka kwa Watu waliokuwa wanatutukana wengine, hapa ndipo dhana ya maendeleo hayana chama inakuja” –Rais Magufuli
RAIS MAGUFULI ‘Lowassa alikuwa Waziri wa Maji ila Mbunge saivi anaomba maji”, BONYEZA PLAYA HAPA CHINI KUTAMA