Leo September 6, 2018 Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Nchini (SIDO) kwa kushirikiana na Mkoa wa Simiyu wameandaa maonyesho ya Kitaifa ya bidhaa za wajasiriamali yatakayofanyika Mkoani Simiyu mwaka huu.
Akizungumzia maandalizi ya maonyesho hayo yanayofanyika kwa mara ya kwanza, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Prof.Sylvester Mpanduji amesema maonesho hayo yatatoa fursa ya kuonyesha na kutangza teknolojia mpya za uzalishaji.
“Maonyesho hayo yatakayofanyika kati ya Oktoba 23 mpaka 28 mwaka huu, yatawaleta wafanyabiashara kutoka nchi za China, India na Ujerumani lengo likiwa kuwahamasisha wajasiriamali nchini na kuwajengea uwezo wa masoko kutoka nchi hizo.” Prof. Mpanduji