Leo August 23, 2019 Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa ameshuhudia meli ya kwanza ikipakia Korosho katika Bandari ya Mtwara ambayo imeuzwa Nje ya Nchi, haya ni matokeo ya ziara aliyofanya baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli.
“Hii ni hatua muhimu ktk kujiandaa na msimu mpya wa korosho unaokaribia, Serikali imelenga kumpa Mkulima bei anayostahili, pili ilikusanya korosho zote na kuweka sehemu salama” Waziri Bashungwa
“Sasa masoko yamepatikana, zoezi la upakiaji kwenye meli limeanza, tumejipanga kusimamia msimu mpya unaokuja uwe na manufaa kwa Wakulima wetu” Waziri Bashungwa