Mteja atafuatiliaje mwenendo wa maombi yake ya kuhama?
Atajulishwa kwa njia ya meseji kuhusu mwenendo wa mchakato wa maombi yake ya kuhama.
Nini kitatokea iwapo maombi ya kuhama yatakataliwa au hayatakamilika?
Mteja atatakiwa kuwasiliana na mtoa huduma wake mpya kupata ufumbuzi wa tatizo.
Iwapo mteja anarejea kwa mtoa huduma wake wa awali, atahitajika kupata laini mpya kutoka kwa mtoa huduma wa awali na hivyo kufanya laini yake ya zamani kutokufanya kazi?
Atahitajika kupewa laini mpya ya simu kila mara anapohama kwenda kwa mtoa huduma mpya kwani laini yake ya zamani haitaweza kutumika kwenyemtandao mpya.
Mteja atahitajika kulipia laini mpya ya simu?
Atapewa laini mpya ya simu na mtoa huduma wake mpya ama bila malipo au kwa malipo kutegemea na utaratibu wa mtoa huduma.
Mteja afanye nini iwapo atakuwa na tatizo au malalamiko?
Anatakiwa kufuata utaratibuu wa kulalamika. Kwanza, awasiliane na mtoa huduma wake mpya ili kupata ufumbuzi. Isipowezekana, au asiporidhika, alalamike kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.