Leo June 26, 2018 Mahakama ya juu nchini Marekani imeidhinisha sera ya Rais Trump ya kuwazuia Raia wanaotoka kwenye mataifa ya Somalia, Iran, Syria na Yemen kuingia nchini Marekani.
Hapo awali Mahakama za ngazi ya chini zilitupilia mbali sera ya hiyo ya rais Trump kwa kile walichokiita kuwa ni kinyume na katiba ya nchi hiyo ya Marekani sababu ambayo imetupiliwa mbali na Mahakama hiyo ya juu.
Katazo hilo la Rais Trump linawakumba pia wakimbizi wote waliokimbia nchi zao kwa sababu mbalimbali kuingia nchini Marekani huku mfumo maalumu wa upekuzi unaoitwa “extreme vetting” unategemewa kuanzishwa.
Mataifa ya Iraq na Chad yalijumuishwa kwenye orodha ya awali lakini yameondolewa katika katazo hilo.
Aidha Kiongozi huyo amesema kuwa sera hiyo inalenga kuzuia Waislamu walio na itikadi kali kuingia nchini Marekani.