Jeshi la Polisi Nchini limeripoti ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia kufikia 43,487 kwa mwaka 2018 kwa ongezeko la matukio 1034 ikilinganishwa na mwaka 2017 kwa matukio ya ukatili wa kijinsia 41,416 ikisababishwa na matukio mbalimbali ya ukatili.
Mkuu wa Dawati la Jinsia Tanzania Marry Nzuki amesema hayo wakati wa Uzinduzi wa dawati la jinsia na watoto Central Polisi Mkoani Kigoma na kwamba hatua hiyo itasaidia kukabilina na vitendo vya ukatili ikiwa wananchi watatumia sehemu hiyo kufikisha matatizo yanayowasibu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma ACP Martini Otieno amesema jamii kuwa na sauti moja na kushirikiana na vyombo vya dola ni hatua ya kukabilina na vitendo vya ukatili na kulea tija hivyo hainabudi kwa jamii kuripoti matukio ya ukatili.