Shirika la RSA Tanzania tawi la Kilimanjaro kwa kushirikiana na na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Kilimanjaro leo wameendesha mafunzo kwa waalimu walezi wa Klabu za Usalama Barabarani kwa wanafunzi.
Lengo la mafunzo hayo elekezi ilikuwa ni kuwajengea uwezo waalimu kuweza kuzisimamia na kuzilea Klabu za Wanafunzi za Usalama Barabarani katika shule zao.
RSA Tanzania chini ya ufadhili wa Foundation for Civil Socities inaendesha Mradi wa Elimu ya Usalama Barabarani Mashuleni (Schools Road Safety Education Project), ambapo mkoani Kilimanjaro shule 11 zimejumuishwa katika mradi huo wa mwaka 1.
Watoa mada wakiongozwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Hamadi Hozza, CLP Maneno Francis, SGT Hilda Mlay na Meja Elituma Samson waliwafundisha waalimu sheria na taratibu za Usalama barabarani na kubwa ni jinsi wanafunzi wanavyotakiwa kuvuka barabarani.
Kwa upande wa mabalozi wa Usalama barabarani (RSA) wakiongozwa na M’kiti wa Mkoa ambae pia ni Naibu Mkurugenzi Elimu kwa umma Khalid Shekoloa na Mratibu Msaidizi wa Mradi Irene Mselem walielezea namna nzima ya jinsi mradi unavyotakiwa kutekelezwa hatua kwa hatua.