Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella amesema kuwa katika Mkoa wake hakuna ugomvi wa kutoelewana kati ya Viongozi wa Wilaya na Watendaji wengine na kuwa Viongozi wote wanaelewana vizuri hali inayopelekea maendeleo kufanywa kwa kasi.
“Kwenye mkoa wa Tanga sijaona mahali ambako kuna mgawanyiko, Viongozi wote wanamshikamano na umoja, nipongeze Wilaya Korogwe mnaonyesha mfano katika hilo” RC Tanga Shigella