Naibu Spika Dr. Tulia Ackson ameamuru Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa kutolewa nje ya ukumbi wa bunge kwa kosa la kuonesha utovu wa nidhamu mbele ya kiti cha Spika.
Tukio limetokea wakati Wabunge wakichangia Azimio la Bunge la kumpongeza Rais Magufuli kwa jitihada na maamuzi mbalimbali na kuwainua wananchi wanyonge hasa wakulima wa korosho, azimio ambalo limeletwa Bungeni na Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu.